Uwanja wa CCM Kirumba, Ssaa 10:00 jioni ni Pamba Jiji FC vs Simba SC mchezo wa NBC Premier League ambayo ni namba 6 kwa ubora.
Kwenye kikosi cha kwanza cha mnyama kiungo Ellie Mpanzu ameanza ikumbukwe kwamba mchezo uliopita dhidi ya Singida Black Stars alianzia benchi na alifunga goli la ushindi akitumia pasi ya Clatous Chama.
Langoni
Mahamadou Kassali.
Mabeki ni Shomari Kapombe, De Reuck, Nickson Kibabage na Ismael Toure. Viungo ni Libasse Gueye, Ellie Mpanzu, Alasane Kante, Yusuph Kagoma na Clatous Chama mshambuliaji ni Anicent Oura.
Wachezaji wa akiba ni Bashiri Salum, Anthony Mligo, Vedastus Masinde, Duchu, Hussen Abel, Naby Camara, Neo Maema, Hussen Mbegu, Semfuko na Morice.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.