Liverpool wamekubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Manchester City katika dimba la Anfield huku mabao ya dakika za lala salama kutoka kwa Bernardo Silva na Erling Haaland yakiiwezesha Man City kupindua meza.
Man City imesogea mpaka alama sita nyuma ya vinara, Arsenal kwenye msimamo wa ligi kuu England wakifikisha alama 50 baada ya mechi 25 huku Liverpool ikisalia nafasi ya sita alama 39 baada ya mechi 25.
FT: Liverpool 1-2 Man City
⚽ 74’ Szoboszlai
⚽ 84’ Silva
⚽ 90+3’ Haaland (P)