Azam FC vs TRA United NBC Premier League ni kituo kinachofuata kwa matajiri wa Dar mchezo ujao wakiwa nyumbani.
Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge itamenyana na wakusanya mapato saa 3:00 usiku Uwanja wa Azam Complex.
Hiyo ni baada ya matajiri hao wa Dar kutoka ugenini kucheza mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Nairobi United wakipata ushindi wa magoli 2-1 na kuvuna pointi tatu kwa mara ya kwanza baada ya mechi mbili kupoteza katika kundi B.
Katika kundi B, Azam FC ni nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya mechi tatu vinara ni Wydad wenye pointi 9 nafasi ya pili ni Maniema FC wenye pointi 6, Nairobi United ipo nafasi ya nne ikiwa haijakusanya pointi baada ya kupoteza mechi zote tatu ilizoshuka uwanjani.
Kwenye ligi Azam FC ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 13 baada ya mechi 7 inakutana na TRA United iliyo nafasi ya 9 na pointi 12 kibindoni.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.