Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji FC ni ushindi kwa mabingwa watetezi kwenye mchezo wa NBC Premier League Januari 27,2026.
Kwenye mchezo wa leo Dodoma Jiji walianza kupata goli la kuongoza kipindi cha kwanza dakika ya 42 kupitia kwa William Edger ambalo lilidumu kwa muda wa dakika 3.
Magoli ya Klabu ya Yanga yamefungwa na Depu dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati na goli la pili dakika ya 61.
Mshambuliaji Prince Dube amefunga goli moja dakika ya 67 likidumu mpaka mwisho wa mchezo kwa timu zote mbili Uwanja wa KMC Complex.
Pointi tatu kwenye mchezo wa leo zimebaki Jangwani huku Dodoma Jiji FC wakipishana na pointi hizo Januari.
Depu amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo kutokana na kiwango ambacho amekionyesha ndani ya uwanja.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.