Januari 23,2026 Al Ahly 2-0 Yanga SC CAF Champions League pointi tatu zimebaki kwa wenyeji ambao wanaongoza kundi B kwa sasa.
Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Borg El Arab huku nyota wa Al Ahly Mahmoud Trezeguet akifunga magoli yote mawili.
Alianza dakika ya 45+3 zikiwa zimesalia sekunde kadhaa kaba ya timu kwenda mapumziko alipofunga goli la kuongoza kwa pigo la kichwa kilichomshinda mlinda mlango Djigui Diarra.
Kipindi cha pili katika dakika ya 75 alipachika goli la pili ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo kwa wababe hawa wawili.
Msimamo wa kundi B upo namna hii
MP
W
D
L
PTS
1. Al Ahly
3
2
1
0
7
2. Yanga SC
2
1
1
1
4
3. AS Far
2
0
1
1
1
4.Kabylie
2
0
1
1
1
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.