Azam FC Yaifunga Simba, Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026

Azam FC wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la NMB Mapinduzi 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC.

Mchezo huo wa robo fainali umechezwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar, ambapo bao pekee la ushindi lilifungwa na Lawi dakika ya 73 ya mchezo, bao lililodumu hadi filimbi ya mwisho.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kuendeleza ubabe dhidi ya Simba SC, ikiwa ni kipigo cha pili mfululizo kwa Wekundu wa Msimbazi kutoka kwa Wanalambalamba. Awali, Azam FC iliifunga Simba kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Desemba 7, 2025.

Kwa matokeo hayo, Azam FC sasa inasubiri mpinzani wake katika fainali ya michuano hiyo inayoendelea kufanyika Zanzibar.

FT: Azam FC 1-0 Simba SC
⚽ Bao: Lawi (dk 73)