Yanga SC 2-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora.
Prince Dube alianza kufunga bao la kwanza kipindi cha kwanza dakika ya 26 kwa mkwaju wa penalti.
Kamba ya pili imefungwa kipindi cha pili Uwanja wa KMC Complex, Desemba 4,2025.
Pacome Zouzoua ametoa pasi mbili za mabao na kufunga mabao mawili hivyo amehusika katika mabao manne ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Bao la Pacome pasi imetoka kwa kiungo Duke Abuya baada ya Fountain Gate kupoteza mpira ukakutana na Zimbwe Jr aliyempa pasi Duke.