KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kina mitambo miwili ya mabao kwenye eneo la kufunga wakiwa na ushindani mkubwa kwa kila mmoja kwenye kucheka na nyavu.
Baada ya mechi 23 safu ya ushambuliaji ya Yanga imetupia jumla ya mabao 61 ikiwa ni timu namba moja kwa kufunga mabao mengi ndani ya ligi msimu wa 2024/25.
Mbali na kufunga mabao 61 kibindoni ina pointi 61 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo ambapo ushindi ni kwenye mechi 20, walitoshana nguvu kwa kugawana pointi mojamoja na JKT Tanzania huku wakipoteza mechi mbili walianza mbele ya Azam FC na Tabora United.
Novemba 7 2024 Tabora United walikomba pointi tatu za Yanga katika mchezo wa mzunguko wa pili walipokutana Aprili 2 2025 ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulisoma Tabora United 0-3 Yanga.
Katika mchezo huo washambuliaji wawili walifunga bao kila mmoja nakufikisha jumla ya mabao 11 kwa kila mshambuliaji ambapo ni Prince Dube na Clement Mzize.
Mzize alifunga bao pekee lakufutia machozi mzunguko wa kwanza dhidi ya Tabora United akawafunga tena kwenye mchezo wa mzunguko wa pili hivyo balaa lake halijapoa.
Dube anashikilia rekodi yakuwa nyota namba mbili kuhusika kwenye mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 18 kafunga mabao 11 na kutoa pasi 7 zinazomfanya ahusike kwenye mabao 18 kati ya 61.
Mchezo ujao kwa Yanga ni dhidi ya Coastal Union unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex Aprili 7 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.