YANGA YATOZWA FAINI YA TSH MILIONI 12 MCHEZO WA DERBY YA KARIAKOO

Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Tsh milioni kumi kwa kosa la kupitia mlango usio rasmi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo wa derby ya Kariakoo uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa na kumalizika kwa Wananchi kuibuka na ushindi wa 1-0 jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mche.

Katika hatua nyingine Wananchi wametozwa faini ya milioni moja kwa kosa la kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo huo kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, adhabu ambayo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Aidha Young Africans Sc imetozwa faini ya Tsh milioni moja kwa kosa la kuwakilishwa na kocha mkuu pekee kwenye mkutano wa Wanahabari kuelekea mchezo huo kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:58 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo inayotaka aambatane na nahodha ama mchezaji mwenye ushawishi kikosini.