BREAKING: GRACE MAPUNDA (TESSA) AFARIKI DUNIA

Habari za kusikitisha zilizotufikia asubuhi hii ya Novemba 2, 2024 zinaeleza kuwa, muigizaji nguli wa Bongo Movies, Grace Mapunda almaarufu Tessa anayeng’ara kwenye Tamthiliya ya Huba amefariki dunia.

GLOBAL TV imezungumza na Meneja Uzalishaji (Production Manager) wa Huba Series aitwaye Saffi ambaye amethibitisha kutokea kwa msiba huo mzito.

Saffi amesema Tessa amefariki dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya Mwananyamala wakati akipatiwa uhamisho wa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na GLOBAL TV, Tessa alieleza namna ambavyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Grace Mapunda au Mama Kawele au Tessa alikuwa muigizaji wa filamu za Tanzania (Swahiliwood), anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuigiza filamu za hisia.

Tessa ametumikia tasnia hiyo kwa takribani miaka 20 kwa umakini mkubwa akiwakilisha uhusika halisi ambapo alionekana kuzipatia mno filamu za aina hiyo.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina!