PATRICK Aussems , Kocha Mkuu wa Singida Black Stars ameweka wazi kuwa bado wapo kwenye mbio za kuwania kombe la Ligi Kuu Bara 2024/25 licha ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Yanga kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa New Amaan ukisoma Singida Black Stars 0-1 Yanga.
Ikumbukwe kwamba kombe la ligi mabingwa watetezi ni Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye ameweka wazi kuwa wanahitaji kulitwaa kwa mara nyingine tena hivyo vita inazidi kuwa kubwa kwa timu hizi uwanjani.
Aussems amesema licha ya kupoteza mchezo wao wa kwanza ndani ya ligi kwa kufungwa na Yanga bado wachezaji wapo kwenye ubora mkubwa na uwezo wa kuendelea kupambania kombe kwa kuwa kupoteza mchezo sio mwisho wa mapambano.
“Kupoteza mchezo dhidi ya Yanga haina maana kwamba tumekosa ubora hapana, uliona namna ambavyo mchezo ulikuwa, tulicheza kwa kiwango kikubwa na hilo ninawapongeza wachezaji kwa kazi nzuri na kubwa.
“Bado tupo imara na malengo ni kuendelea kupambana kwa ajili ya kombe huku mpango mkubwa ukiwa kumaliza ndani ya tatu bora kwenye ligi inawezekana na tupo tayari.”
Singida Black Stars baada ya kucheza mechi 9, kibindoni ina jumla ya pointi 22 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.