>

KAGERA SUGAR YAPOTEZA MBELE YA YANGA, MAXI, MZIZE WAA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga wamefungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza wakiwa ugenini.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba umesoma Kagera Sugar 0-2 Yanga wakisepa na pointi tatu mazima msimu wa 2024/25.

Maxi Nzengeli alipachika bao la ufunguzi dakika ya 25 akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Kagera Sugar baada ya pigo la faulo kuanzishwa na Yanga haraka.

Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo Yanga ilipachika bao kupitia kwa Clement Mzize ambaye alianzia benchi kwenye mchezo wa leo na kapachika bao hilo dakika ya 88 kwa mguu wa kulia.

Mzize aliingia dakika ya 64 akichukua nafasi ya Prince Dube na Clatous Chama naye aliingia akichukua nafasi ya Pacome.