>

FOUNTAIN GATE YAWAPIGA MKWARA SIMBA

BAADA ya ushindi wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, Fountain Gate wameipiga mkwara timu iliyowafunga katika mchezo wa kwanza ambayo ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Agosti 29 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 0-2 Fountain Gate huku Namungo wakikosa penalti dakika ya 25 kwenye mchezo huo ambayo waliipata kutokana na beki wa Fountain Gate kudaiwa kucheza faulo ndani ya 18.

Mabao ya Fountain Gate yalifungwa na Edger William dakika ya 30 na bao la pili lilifungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 45 hivyo kazi iligotea hapo kwa mabao hayo kudumu mpaka mwisho wa mchezo.

Ikumbukwe kwamba Fountain Gate mchezo wa kwanza msimu wa 2024/25 ilikuwa Simba 4-0 Fountain  Gate ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge.

Issa Liponda, Ofisa Habari wa Fountain Gate amesema kuwa wamejitafuta na kujipata hivyo hawana tatizo na timu yoyote ile wakiomba kurudiana na timu iliyowafunga ya Ubaya Ubwela ambayo ni Simba.

“Tumejitafuta na sasa tumejipata, tunaomba kurudiana na ile timu ya ubaya ubwela, hakika tunawakada nyingi hatuna mashaka tuna wachezaji weye uwezo na wanajituma.”