Klabu ya PSG imeshinda mbio ya kuwania saini ya kiungo Joao Neves baada ya kukamilisha dili hilo kwa dau la Euro milioni 70 akitokea Benfica ya Ureno. Neves (19) raia wa Ureno amesaini mkataba wa miaka mitano.
Baada ya kuwika na miamba hiyo ya Ureno msimu uliopita Manchester United na PSG walijikuta kwenye vita kali huku miamba hiyo ya England ikitolewa nje huku PSG ikishinda vita hivyo.
Wakati Mashetani Wekundu wakigugumia maumivu ya kuikosa saini ya Neves, hatua hiyo inaweza kuwa ‘afueni’ kwao kwani kuondoka kwa Mreno huyo kunaweza kufungua njia ya PSG kumwachia kiungo wa Manuel Ugarte kwenda Old Trafford.
Ripoti za hivi karibuni zinadai kuwa PSG itakuwa tayari kumtoa Ugarte kwa mkopo ikiwa watapata dili la Neves.