Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania ( TPLB ), Almas Kasongo ameeleza kuwa msimu ujao watatoa adhabu kwa maofisa habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira.
“ Kuna Muda unamsikiliza Ofisa Habari wa timu na kujiuliza, huyu ni kiongozi wa timu au mchekeshaji? Niseme tu ndugu zangu, msimu ujao tutadili na watu hawa kwa kuwapa adhabu “
– Almas Kasongo, CEO Bodi ya Ligi kuu Tanzania.