BAADA YA UTAMBULISHO WA LAMECK LAWI KLABU YA SIMBA, UONGOZI WA COASTAL UNION WAFUNGUKA MAZITO

Baada ya utambulisho wa Lameck Lawi kama mchezaji mpya wa klabu ya Simba, Uongozi wa Coastal Union kupitia kwa Afisa Habari wake Abbas El Sabri umefunguka kwamba hautambui utambulisho huo na kubainisha kwamba hizo ni taarifa za kufurahisha na kuchekesha za mitandaoni.

“Siku hizi mitandaoni kuna mambo mengi sana wakati mwingine kuna mambo ya kufurahisha kuchekesha kwa hiyo ndio Dunia ya sasa ilivyo.”

“Hizo taarifa hata sisi ndio tunaziona mitandaoni lakini ukweli ni kwamba Lameck Lawi bado ni mali ya Coastal Union na ni mchezaji halali wa Coastal Union.”

“Mimi kama Afisa Habari wa Coastal Union nasema Lameck Lawi hajauzwa timu yoyote, ni Mali ya Coastal Union na bado tuna mipango naye.” — Abbas El Sabri

“Ilipokuja ofa tuliwapa taratibu za kufuatia na namna ya kufanya kama wanamuhitaji sasa sijui ni nini kimewafanya wasifanye vile sisi tunataka kwa hiyo na sisi baada ya kuona pengine hawana nia tena tukakaa na kuamua mengine.” — Abbas El Sabri