BIASHARA UNITED MARA WAMEFIKA MKOANI TABORA WADAI KUPOKELEWA KWA KIPIGO

Biashara United Mara wamefika mkoani Tabora na kupokelewa kwa kipigo asubuhi hii wakati wanaenda kwenye pre match Meeting.

Technical director Omary Madenge imeshambuliwa sana hali yake ni mbaya lakini pia amenyang’anywa baadhi vitu alivyokuwa navyo.

Lakini pia viongozi wawili wa Biashara United Mara hawajulikani walipo, wamechukuliwa na kupelekwa kusikojulikana.

Kwasasa gari iliyovamiwa na kushambuliwa ipo Polisi lakini hakuna ushirikiano wowote wa Polisi , taarifa zinaonesha kuwa hakuna ulinzi wowote ambao Biashara United watapewa.

RPC Tabora anaombwa kusimamia ulinzi wa watanzania katika michezo huu