ZAIDI YA BILIONI 283 ZIMETOLEWA WIZARA YA MICHEZO

NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema kuwa zaidi ya bilioni 283 zimetolewa kwenye wizara ya michezo ikiwa ni mara 8 zaidi ya bajeti ya awali.

Mwinjuma ameweka wazi kuwa shukrani zote ni kwa mwanamichezo namba moja Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye jitihada zake za kuunga mkono maaendeleo ya michezo zinaendelea.

Hayo aliyasema kwenye uzinduzi wa kitabu cha Yanga Juni 15 2024 ambapo Mwinjuma alikuwa miongoni mwa wageni waliohudhuria tukio hilo.

Kiongozi huyo amesema: “Nichukue nafasi hii kumshukuru mwanamichezo namba moja Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake kuunga mkono maendeleo ya michezo nchi hii. Mheshimiwa Rais ametoa zaidi ya bilion 283 kwenye wizara ya michezo, hii ni zaidi ya mara 8 ya bajeti ya awali.

Kuhusu suala la uzinduzi wa kitabu Mwinjuma amesema:“Niseme ukweli, huwa napenda sana kuja kwenye shughuli za Yanga, kwa sababu ya maendeleo na hatua wanayopiga. Mwaka jana walikuja na Documentary, mwaka huu wamekuja na kitabu, hatuwezi kujua tunakokwenda kama hatujui tulipotoka.

“Hii ni hatua kubwa sana kwenye maendeleo ya timu. Nimpongeze sana GSM na Injinia Hersi kwa juhudi zao ambazo wanazifanya matokeo yanaonekana.”