Dirisha la Usajili (FIFA Connect) kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC (NBCPL), Championship League (CL), First League (FL) na Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) msimu wa 2024/2025 linafunguliwa kesho Jumamosi Juni 15, 2024 na litafungwa Agosti 15 2025.
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limezitaka Klabu kufanya usajili na uhamisho wa wachezaji huku ikisisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Aidha usajili na uhamisho wa wachezaji kwa dirisha dogo utafunguliwa Desemba 16, 2024 na kufungwa Januari 15, 2025.