YANGA KUJA NA JAMBO HILI KUBWA

JAMBO lingine kubwa linakuja kutoka kwa Yanga mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 wakidhaminiwa na kampuni ya SportPesa.

Jambo hilo ni uzinduzi wa kitabu cha Yanga kinachotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi Juni 15 uongozi wa Yanga umebainisha kwamba umekusanya mengi ya muhimu bila kuacha chochote.

Ipo wazi kwamba kwa msimu wa 2023/24 Yanga imetwaa taji la Ligi Kuu Bara, CRDB Federation Cup na ilitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa jambo hilo la uzinduzi wa kitabu limekuwa likisubiriwa kwa shauku kubwa limefanyika kwa umakini mkubwa ili kuwapa yale yaliyo muhimu mashabiki na wanachama.

“Ni jambo la kihistoria tunakwenda kufanya Yanga ni klabu yenye miaka 89 na kuna mengi ambayo wanachama na mashabiki wanahitaji kuyajua kazi hii tumeanza kuifanya miezi saba iliyopita na safari hii hatujaacha chochote.

“Mashabiki na Wanachama wanahitaji kupata kile kilicho bora na tunaamini kupitia hiki kitabu kuna simulizi nyingi nzuri watakutana nazo ambazo zinaeleza namna ilivyokuwa tangu awali mpaka sasa.”