MANGUNGU: MO DEWJI NI MWANASIMBA JASIRI

Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amewajibu Wanasimba wanaodhani kuwa hana maelewano na Mwekezaji Mo Dewji kuwa “Nani kawaambia? Anasema hana chuki na Mo Dewji na kuongeza kuwa anayemsimanga Mo siyo mwana Simba ni kiumbe kingine,

“Mimi simchukulii Mo kama muwekezaji pekee, namchukulia kama mtu jasiri ambaye anatumia nguvu na pesa zake kuisaidia Simba, hata hiyo memorandum tunayoizungumzia hapa ni yeye na moyo wake amechagua kufanya, ingekuwa mtu mwingine angesubiri hadi mchakato ukamilike”

“Sisi tunamchukulia kama mwanasimba jasiri aliyechagua kuisaidia Simba” – Mangungu