MANGUNGU: ISSA MASOUD HANA MAMLAKA YA KUITISHA MKUTANO

“Sisi tunajuana tangu tunakua , haiwezekani mtu ambaye hana nasaba na Simba akawa ndani ya klabu , mimi nimepata kadi yangu ya uwanachama mwaka 1993”

“Niulize sasa , Kwahiyo tangu mwaka 1993 tuseme nilijipanga nije kuwa mwemyekiti wa Simba ili nije kuihujumu ? anayenishutumu mimi nahujumu Simba yeye hata kadi ya uanachama hana”

Wakati anajibu kuhusu maoni ya mdau aliyehoji viwango duni vya baadhi ya wachezaji wanaosajiliwa na Simba Mangungu amesema

“Yeye amezungumzia wachezaji wawili Sawadogo na Jobe , bahati mbaya Sawadogo wakati anakuja pre season aliumia , lakini alikuwa anatoka kwenye timu yao ya Taifa sio mchezaji wa kiwango kidogo”

“Mimi ninachosema hapa atokee mtu anipe timu 5 ambazo wamesajili na wachezaji wote waliosajiliwa wamefanya vizuri,Wallah mimi wala sisubiri kitu ,kesho najiuzulu”

Majibu ya Murtaza Mangungu kuhusu kuihujumu Simba SC