JUVENTUS YAMTEUA THIAGO MOTTA KUWA KOCHA MPYA

Klabu ya Juventus ya Serie A imethibitisha kumteua mkufunzi Thiago Motta kuwa kocha mkuu klabuni hapo kwa mkataba wa miaka mitatu mpaka Juni 2027.

“Ninayo furaha kuanza ukurasa huu mpya katika klabu bora kama Juventus, asante kwa imani yenu na ninaweza kuhakikisha nitajitolea kuwafanya mashabiki wa Juventus wajivunie”. — Mota

Mota (41) raia wa Italia alikuwa mmoja wa makocha bora barani Ulaya msimu wa 2023/24 akiiongoza Bologna kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.