Mkongwe wa mpira wa kikapu wa Marekani Jerry West (86), amefariki dunia.
West alicheza mpira huo kwa miaka 14 na kucheza katika fainali 9 za NBA chini ya timu ya Lakers ya Los Angeles, na kushinda mara moja mwaka 1972.
West atakumbukwa kwa umahiri wake na zaidi kwa alama ya kudumu aliyoiacha kwenye nembo ya NBA ambayo iliundwa kwa kufuatilia picha yake.