AZAM FC NA HESABU ZAO

YUSUPH Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa msimu wa 2023/24 ulikuwa na ushindani mkubwa na kila mchezaji alikuwa akitimiza majukumu yake.

Ni wazi kuwa Azam FC inaungana na Yanga kupeperusha bendera ya Tanzania Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ambapo ilimaliza ikiwa na pointi 69 baada ya kucheza mechi 30 ndani ya ligi ikiwaacha Simba nafasi ya tatu wakiwa na pointi 69tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mchezo wa funga kazi kwa Azam FC ilikuwa dhidi ya Geita Gold walikomba pointi tatu Mei 28 kwa ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini.

Dabo amesema: “Ni msimu uliokuwa na ushindani mkubwa, pongezi kwa wachezaji wamefanya kazi kubwa na tunawapongeza.Mashabiki walikuwa pamoja nasi kwenye mechi ambazo tulikuwa tunacheza.

“Haikuwa rahisi kwani ushindani ulikuwa mkubwa lakini tulikuwa tunapambana kupata matokeo kwenye mechi ambazo tulikuwa tunacheza ndani ya uwanja.”

Mchezo ujao kwa Azam FC ni funga kazi msimu wa 2023/24 fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Yanga.