FEI TOTO AFUNGUKIA TUZO YA AZIZ KI

MFUNGAJI namba moja kwa wazawa Feisal Salum anayetimiza majukumu yake ndani ya Azam FC amempa pongezi mfungaji bora wa ligi msimu wa 2023/24 ndani ya ligi.

Ikumbukwe kwamba vita ya kiatu cha ufungaji bora ilikuwa kali kati ya Fei aliyemaliza msimu akiwa na mabao 19 huku Aziz KI akitupia jumla ya mabao 21.

Nyota hao wawili kwenye mchezo wa mzunguko wa 29 kila mmoja aligotea kwenye mabao 18 na mechi ya mzunguko wa 30 ilikuwa ni mwisho wa ubishi kwa kila mchezaji kutimiza majukumu yake.

Mwisho, Aziz KI alifunga hat trick mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Azam Complex na Fei alifunga bao moja Uwanja wa Nyankumbu dhidi ya Geita Gold.

Feisal amesema: “Ilikuwa ni ushindani mkubwa kwa namna ilivyotokea ninampongeza Aziz KI kwa kuwa mfungaji bora. Kikubwa ilikuwa ni kutafuta matokeo ya timu kwetu imekuwa hivyo na tunafurahi.

“Tuna nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ni hatua kubwa kwetu tunaamini kwamba tutafanya vizuri na wakati ujao tutarejea tukiwa imara.”