ISOME AZIZ KI HAKIKISHA

MABAO 21 kibindoni mwamba Aziz KI kakamikisha akiwa ni mfungaji bora msimu wa 2023/24 ambao umegota mwisho leo Mei 28 2024.

Kwenye tuzo ya ufungaji bora hakikisha jina linasoma Aziz KI kwa kuwa amefanya kazi yake kwa ushirikiano mkubwa na wachezaji wengine ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ushindi wa mabao 4-1 waliopata Yanga mbele ya Tanzania Prisons umewapa pointi tatu nyingine huku Azam FC ikigotea nafasi ya pili na pointj 69.

Feisal Salum ni namba mbili kwa wakali wa kutupia akiwa na mabao 19 msimu wa 2023/24.

Mbali na kufunga nyota huyo raia wa Burkina Faso ambaye ni chaguo la kwanza la kocha ametengeneza jumla ya pasi za mabao 8 kwenye kikosi hicho.

Mkali wa mapigo ya penalti akiwa amefunga penalti tatu na kwenye mapigo huru hana bahati mbaya kwa kuwa bao moja kati ya matatu ambayo kafunga mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni pigo huru.