SIMBA: HII IMEISHA, MIPANGO INAANZA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa msimu wa 2023/24 umegota mwisho hivyo ni hesabu kwa ajili ya msimu mpya 2024/25.

Kete ya mwisho ya funga msimu ilikuwa ni Mei 28 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 JKT Tanzania.

Hivyo Simba imekomba pointi sita mazima mbele ya JKT Tanzania kwa kuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa JKT Tanzania 0-1 Simba, bao lilifungwa na Clatous Chama.

Mabao ya Simba dhidi ya JKT Tanzania mzunguko wa pili ni mali ya Saido Ntibanzokiza dakika ya 88 kwa mkwaju wa penalti na Willy Onana dakika ya 90.

Ni pointi 69 Simba imegotea ikiwa nafasi ya tatu tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Azam FC iliyo nafasi ya tatu.

Kocha huyo amesema: “Hii imeisha na niliweka wazi mwanzo kuwa haijafika mwisho mpaka ifike mwisho, kila mmoja alikuwa na malengo yake lakini mwisho imefahamika nani ameongoza nani yupo nafasi ya pili.”

Mechi 9 kaongoza ambazo ni dakika 810 katika mechi hizo kaambulia sare mechi mbili ilikuwa Kagera Sugar 1-1 Simba na mchezo wa kwanza kukaa benchi ilikuwa Namungo 2-2 Simba.