MASHUJAA KUONYESHA USHUJAA KWA YANGA

BENCHI la ufundi la Mashujaa limebainisha kwamba lipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya vinara wa ligi ambao ni Yanga.

Mchezo huo wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma kwa wababe wote wawili kusaka pointi tatu muhimu.

Ipo wazi kuwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Mashujaa hivyo pointi tatu zilikuwa mali ya Yanga.

Kocha Abdallah Barres wa Mashujaa amebainisha kwamba wanatambua ugumu wa mchezo dhidi ya Yanga lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu.

“Mchezo utakuwa mgumu hilo tunatambua lakini tuawaheshimu Yanga na tunatambua ni wapinzani wagumu. Makosa ambayo yalitokea kwenye mechi zetu ambazo zimepita tumefanyia kazi.”