Home Sports BINGWA WA MUUNGANO ATAJWA NA WIZARA YA MICHEZO

BINGWA WA MUUNGANO ATAJWA NA WIZARA YA MICHEZO

NAIBU Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, maarufu kama FA amesema kuwa bingwa wa leo kwenye mchezo wa fainali wa Muungano ataandika rekodi ya kuwa bingwa mpya baada ya mashindano hayo kurejea.

FA amesema hayo kwenye uzinduzi wa mashindano ya Dar Youth Cup yaliyoandaliwa na  Bull Football Academy kituo cha kukuza vipaji watoto ikiwa ni mwaka wa tano yaliyofanyika Viwanja vya JK Park.

FA amesema: “Ligi ya Muungano ni kitu ambacho kimesimama kwa muda mrefu lakini kwa sababu sasa hivi tunasherehekea miaka 60 ya Muungano tukaona ni lazima ligi irejee, niamini mimi kwa ajili ya mechi ya leo timu bora na ishinde,”

Leo Aprili 27 Uwanja wa New Amaan Complex mchezo wa fainali ya Muungano unatarajiwa kuchezwa kati ya Azam FC dhidi ya Simba ambazo zimetinga katika hatua ya fainali.

Previous articleLIGI KUU BARA: YANGA 1-0 COASTAL UNION
Next articleSIMBA MABINGWA WA MUUNGANO 2024