Home Sports YANGA YAPETA SPORTPESA DABI

YANGA YAPETA SPORTPESA DABI

YANGA wanaondoka na faida ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Fountain Gate kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ni kwenye SportPesa Dabi Yanga wameibuka wababe kwa kukomba pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo baada ya dakika 90.

Joseph Guede ameandika rekodi ya kufunga mabao mawili dakika ya 41 na dakika ya 68 huku bao moja likifungwa na Aziz KI dakika ya 66.

Singida Fountain Gate ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 22 msimu wa 2023/24.

Ikumbukwe kwamba Singjda Fountain Gate wamepoteza pointi zote sita mbele ya Yanga, mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Yanga 2-0 Singida Fountain Gate.

Yanga inafikisha jumla ya pointi 55 baada ya kucheza mechi 21 ndani ya ligi kituo kinachofuata ni Kariakoo Dabi dhidi ya Simba, Aprili 20 2024.

Previous articleKAKOLANYA ATOROKA KAMBINI SINGIDA FOUNTAIN GATE
Next articleKasino ya Fruit Salad 100 Ushindi 95.06%