Home Sports KAKOLANYA ATOROKA KAMBINI SINGIDA FOUNTAIN GATE

KAKOLANYA ATOROKA KAMBINI SINGIDA FOUNTAIN GATE

UONGOZI wa Singida Fountain Gate umebainisha kwamba kipa wao namba moja Beno Kakolanya ametoroka kambini.

Taarifa iliyotolewa na Singida Fountain Gate inayoshiriki Ligi Kuu Bara imebainisha kuwa kipa huyo ametoroka muda mfupi wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

“Klabu ya Singida Fountain Gate inasikitishwa na kitendo cha mchezaji wetu Beno Kakolanya kutoroka kambini tukiwa tunakabiliwa na mchezo muhimu kabisa dhidi ya Yanga.

“Kitendo hiki kinaleta maswali mengi hasa ukizingatia kwamba Beno ni mchezaji mzoefu na mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa na timu ya taifa ya Tanzania. Tunaendelea kufuatilia taarifa zakena wachezaji wetu wengine wowote ambao wataonekana kuihujumu timu yetu na kwenye mechi nyingine zinazofuata,”.

Previous articleAnza Jumapili yako na Ukiwa na Meridianbet
Next articleYANGA YAPETA SPORTPESA DABI