Home Sports SIMBA YAPIGA HESABU NDEFU KWA AL AHLY KIMATAIFA

SIMBA YAPIGA HESABU NDEFU KWA AL AHLY KIMATAIFA

UONGOZI wa Simba umebainisha kwamba hesabu kubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zote mbili za kimataifa hatua ya robo fainali kwa kuanza na kazi Uwanja wa Mkapa dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Ipo wazi kwamba Al Ahly watakuwa wapinzani wa Simba kwenye hatua ya robo fainali wakipata ushindi dhidi yao watatinga nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi 29 Uwanja wa Mkapa ambapo Simba watakuwa nyumbani kwenye mchezo wa mkono wa kwanza na ule wa pili itakuwa ugenini.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa na wapinzani wao sio wa kuwabeza wataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa na maandalizi yanaanza mapema.

Kikubwa ni kuona kwamba jambo la kwanza kuwa kwenye hatua ya robo fainali limekamilika sasa mpinzani wetu tumetambua kazi kubwa ni kupata matokeo kwenye mechi zetu zilizobaki.

“Hakuna ambaye hapendi kufika hatua ya nusu fainali lakini ili ufike hapo ni lazima uanzie hapa kwenye hatua ya robo fainali na kazi yetu lazima iwe kupambana kwa nguvu kubwa hili linawezekana mashabiki tuwe pamoja,”.

Previous articleHII HAPA SIRI YA MWAMBA AZIZ KI
Next articleAZAM FC YAREJEA CHIMBO