Home Sports AZAM FC YAREJEA CHIMBO

AZAM FC YAREJEA CHIMBO

KIKOSI cha Azam FC kinachofundishwa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo kimerejea chimbo kwa maandalizi ya mechi za ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.

Azam FC inaingia kwenye rekodi ya timu mbili ambazo zimepata ushindi mbele ya Yanga inayofundishwa na Miguel Gamondi katika mechi za ligi.

Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa watetezi wamekuwa kwenye mwendo bora katika msimu wa 2023/24 wakipoteza mechi mbili pekee.

Ilikuwa dhidi ya Ihefu ugenini iliposhuhudia ubao ukisoma Ihefu 2-1 Yanga na mchezo wa pili Mzizima Dabi, Azam FC 2-1 Yanga.

Kwenye mchezo huo kiungo Feisal Salum aliyekuwa mali ya Yanga alipachika bao la ushindi dakika ya 52 akitumia pasi ya Sopu ndani ya 18 Uwanja wa Mkapa.

Bao la Yanga lilifungwa na Clement Mzize ambaye alitumia pasi ya Aziz KI aliyefunga mabao matatu kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Previous articleSIMBA YAPIGA HESABU NDEFU KWA AL AHLY KIMATAIFA
Next articleSIMBA YAIATAKA NUSU FAINALI, KUBADILIKA NA AL AHLY