Home Sports HII HAPA SIRI YA MWAMBA AZIZ KI

HII HAPA SIRI YA MWAMBA AZIZ KI

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Aziz KI raia wa Burkina Faso ameweka wazi kuwa ushirikiano mkubwa kutoka kwenye benchi la ufundi pamoja na wachezaji ni nguzo kubwa kupata mafanikio katika mechi wanazocheza.

Ipo wazi kwamba Aziz KI ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga akiwa na mabao 13 idadi hiyo ni sawa na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum.

Kwenye mchezo wa kisasi dhidi ya Ihefu uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ubao uliposoma Yanga 5-0 Ihefu alihusika kwenye mabao manne, alifunga bao moja na kutengeneza jumla ya pasi tatu za mabao ikiwa ni rekodi ya hat trick ya pasi kwake msimu wa 2023/24.

Kiungo huyo amesema: “Kila mmoja anapenda kuona tunakuwa na furaha ndani ya timu hilo lipo wazi tunashirikiana vizuri kuanzia benchi la ufundi, wachezaji kila mmoja anatimiza majukumu yake.

“Viongozi nao wapo bega kwa bega na sisi usisahau na mashabiki hawa wamekuwa pamoja nasi kwenye mechi zote nyakati zote tunaendelea kupambana ili kupata matokeo chanya kwenye mechi zetu zote,”.

Previous articleMAGAZETI YA MICHEZO LEO MACHI 26, 2024
Next articleSIMBA YAPIGA HESABU NDEFU KWA AL AHLY KIMATAIFA