Home International YANGA KUCHEZA KWA KUWASHAMBULIA WAARABU

YANGA KUCHEZA KWA KUWASHAMBULIA WAARABU

MPANGO kazi kwa Yanga kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakuwa ni kucheza kwa kushambulia kwa kuwa ni sanaa inayopendwa na benchi la ufundi.

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kuwa anapenda kuona timu ikicheza na sio kujilinda muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwapa matokeo chanya.

Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa wa Cairo ambao ni wa hatua ya makundi.

Gamondi amesema: “Mimi sio kocha ambaye napendelea kuzuia timu kwa kukaba dakika 90, mpira kwangu ni kama tamasha la maonesho nafikiri mkinifuatilia utagundua niliwahi kuja hapa zamani, soka langu ni la kushambulia na siwezi kubadilisha sanaa ya soka langu bila kujali nakutana na mpinzani wa namna gani nitaheshimu wapinzani wangu lakini kwangu heshima sio hofu.

“Kila ninapoandaa timu naanda timu kushinda na si vinginevyo mimi ninawaamini wachezaji wangu kwa kiasi kikubwa nimewahi kucheza na Al Ahly nikiwa na Platnumz Stars na kuwa klabu ya kwanza kuifunga Al Ahly kutoka Afrika Kusini, kwahiyo sina wasiwasi wala hofu ya kucheza dhidi ya timu kubwa,”.

Previous articleISHU YA UBUTU WA SAFU YA USHAMBULIAJI WAMKASIRISHA BENCHIKHA
Next articleNHIF: HOSPITALI BINAFSI ZINAZOSITISHA HUDUMA ZINAKIUKA MKATABA, TUNASAJILI VITUO VIPYA