MUDATHIR NA JOB WAMEFANYA HAYA YANGA

MIAMBA wawili ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2023/24 wamefanya yao kwa kuandika rekodi za kuwa nyota wa kwanza kufunga katika mechi za mwanzo kwa kila mzunguko.

Kasi ya kiungo Mudathir Yahya kutoka mzunguko wa kwanza imeendelea mpaka mzunguko wa pili akifanya yake ndani ya uwanja.

Ikumbukwe kwamba Mudathir alifunga mabao kwenye mechi za ligi kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji na Mashujaa alipofunga dakika ya 85 katika mechi hizo.

Katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Dodoma Jiji huku bao likifungwa kipindi cha pili dakika ya 85 na pointi zikabaki Jangwani.

Mchezo dhidi ya Mashujaa bao la dakika ya 85 kutoka kwa Mudathir lilitosha kuipa Yanga ushindi wakakomba pointi tatu ubao uliposoma Yanga 2-1 Mashujaa ya kutoka Kigoma.

Nyota huyo kwenye mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya KMC ubao wa Uwanja wa Jamhuri Morogoro uliposoma KMC 0-3 Yanga alifunga mabao mawili huku bao moja likifungwa na Pacome.

Anakuwa ni mchezaji wa kwanza kufunga bao ndani ya mzunguko wa pili katika kikosi cha Yanga huku bao la kwanza mzunguko wa kwanza likifungwa na Dickson Job.