SANAMU la NYERERE LAVUNJA MBAVU WATU IKULU – ”MADARAKA NYERERE AMESEMA YULE ni BABA YAKE”…

Serikali ya Tanzania kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa, imesema ilifuata maelekezo ya Kitaalamu wakati wa uandaaji wa Sanamu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. #Nyerere

Balozi Shaibu amesema vigezo vilivyotumika ni kumlenga Nyerere wa Miaka 60 hadi 80 wakati akiwa ‘Active’ katika mapambano ya kusaidia kupatikana kwa Uhuru na Maendeleo katika Nchi za Kusini mwa Afrika pamoja na uthibitisho wa Mtoto wake, Madaraka Nyerere

Ameongeza “Taratibu za kitaalamu zinasema unapotengeneza Sanamu unatakiwa uipatie angalau kufikia 75%, ambapo Sanamu ya Nyerere ya #AddisAbaba matokeo yake yamekuwa 92%, na Waziri wa Utamaduni na Michezo alitoa ufafanuzi wa kina juu ya hili”

Kauli ya Serikali inakuja wakati kukiwa na mjadala wa baadhi ya Wadau wanaosema Sanamu hiyo haifanani na mwonekano wa Sura ya Muasisi huyo wa Taifa