NDANI ya Februari kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha kina kazi kubwa ya kusaka pointi tatu ambazo wapinzani wao wanazihitaji pia.
Kigongo cha kwanza kinatarajiwa kuwa leo Februari 3 ugenini mwisho wa reli Kigoma kwa kupambana dhidi ya wenyeji wao Mashujaa Uwanja wa Lake Tanganyika.
Katika mchezo wa leo Simba imemuongeza kiungo Clatous Chama ambaye alikuwa nje kwa muda mrefu kutokana na adhabu ambayo alikuwa nayo kwa sasa akiwa amesamehewa.