Home International HUYU HAPA MRITHI WA MIKOBA YA KLOPP LIVERPOOL

HUYU HAPA MRITHI WA MIKOBA YA KLOPP LIVERPOOL

JURGEN Klopp ataondoka mwishoni mwa msimu. Hili siyo suala la mjadala tena. It is true, Ni kweli kabisa kuwa ataondoka. Mjadala umewefungwa.Mjadala wa sasa ni nani haswa anaepaswa kuchukua mikoba yake?! Mtazamo wangu mimi uko kwa msaidizi wa Klopp. Pepjin Lijnders. Huyu ndie naemuona kama mrithi sahihi wa Klopp. Viashiria vipo vingi na tunaweza kujadili pamoja.

Awali niliwaeleza kuhusu utamaduni wa Kocha wa Liverpool kuzalishwa kupitia Boot Room Tradional enzi za akina Bill Shankly.

Shankly wakati anaondoka 1974 ilikua ni mshtuko mkubwa kwa Liverpool. Na kukawa na mipango ya kuchukua mrithi wake kutoka nje ya Liverpool.

Majina ya Jack Charlton na Bobby Robson yalitajwa kama outiside successors wa Shankly. But Klabu ikasema maneno haya, “ We simply dont want to lose on what Shankly had built in his 15 years. We want continuity” Klabu ilitaka kuendeleza project ambayo tayari imeanzishwa na Shankly.

Na hii kauli ndio tutaitumia kumpata mrithi wa Klopp. Kuja kwa kocha kutoka nje ya Boot Room maana yake tungeanza upya na Klabu haikutaka hilo. Ndipo msaidizi wa Klopp, Bob Paisley akachukua timu.

Tunavyozungumza, Paisley ndo the most decorated manager in Liverpool history. Na ndio kocha wa kwanza kushinda mataji matatu ya Ulaya. Weka nukta hapo!

Turudi hapa: Nikaandika pia ni kana kwamba Klopp nae alianzisha new day boot room. Na hapa ndipo nataka tujadili kwanini namuona Lijnders kama Bob Paisley mpya.

Katika miaka nane hii ya Klopp, miaka hii mitatu ni kama alianza kumuandaa Lijnders kuchukua nafasi yake. Alianza kumpa power kubwa ndani ya Timu.

Mosi alimpa role ya FA na Carabao. Lijnders ndie alikua anaenda kwenye press zote za mashindano haya. Na hata vikosi akawa anapanga yeye.Jambo ambalo huwezi kuliona kwa timu nyingine.

Pili Klopp akampa nafasi kubwa ya kupendekeza wachezaji wa kusajiliwa na Klabu. Darwin Nunez, Luis Diaz, Diogo Jota, Cody Gapko na Fabio Carvalho zilikua signings za Lijnders.

Sidhani kama kuna kocha msaidizi wa timu zingine mwenye nafasi kama hii. Kwahiyo nashawishika kusema kwamba Klopp alimuandaa Lijnders kumrithi. Tunahitaji kocha wa kuendeleza project.

Ameandika James anapenda kujiita Billy Shankly

Previous articleCheza Sloti ya GOLD OASIS Kasino Bora Meridianbet
Next articleJEMBE JIPYA YANGA LAWATAJA AZIZ KI NA PACOME