Home International IVORY COAST NI DARASA TUJIFUNZE

IVORY COAST NI DARASA TUJIFUNZE

KAMA ungekuwa hapa Abidjan ungeweza kunielewa, hakika ni zaidi ya msiba. Nilifika hapa kutokea San Pedro kwa nia ya kuwaona wenyeji lakini wametolewa.

Wakati tukiingia Abidjan, bendera na jezi za wenyeji zilitamba kila sehemu na ilionekana kupoteza haikuwasumbua au kuwakatisha tamaa.

Wamepoteza kwa mabao manne na kutolewa, hakika ni zaidi ya MSIBA na ukiwaona walivyo utaona huruma.

Nikawaza ingekuwa nyumbani halafu sisi ndio wenyeji na tuna wachezaji kama wa Ivory Coast na maandalizi kama yao halafu katika mechi 3 za kundi tupoteze mechi 2…tutolewe…mhh!

Ok, wageni hawapo sasa lakini natamani licha ya kwamba wadau wengi wa mpira wa Tanzania hawapo hapa lakini LAZIMA WAJIFUNZE…

Kuna jambo limewatokea Ivory Coast lakini ukweli hawakuwa na timu imara saizi ya Afcon na sasa mpira wa Afrika umebadilika.

Wewe ni shabiki, jifunze, viongozi wajifunze, wachezaji wajifunze ili tuutambue mpira vizuri kwa kuwa hata wao Ivory Coast WAKILALAMIKA sasa ni kazi bureeee….

Inabidi warudi nyuma WAJIPANGE lakini kwanza lazima WAJIFUNZE…

Ameandika Jembe.

 

Previous articleAMEACHIWA MSALA HUYU HAPA ISHU YA USAJILI SIMBA/ TAHARUKI BALEKE NA PHIRI
Next articleMKALI WA KUCHEKA NA NYAVU HUYU HAPA AFCON