Home Sports GUEDE: NAKUJA KUWAPA FURAHA YANGA

GUEDE: NAKUJA KUWAPA FURAHA YANGA

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Joseph Geude raia wa Ivory Coast hatimaye amefunguka kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo kupitia dirisha dogo lililofungwa Jumanne ya wiki hii.

Mshambuliaji huyo amekuja kuchukuwa nafasi ya mshambuliaji Hafiz Konkoni ambaye ametolewa kwa mkopo kwenda katika klabu ya Dogan Birligi ya nchini Cyprus.

Yanga kupitia dirisha dogo la Usajili limefanya usajili wa wachezaji wawili tu wakimataifa ambao ni winga Mghana Augustine Okrah na mshambuliaji Joseph Guede huku kwa wazawa akiwa ni Shekhan Hamisi pekee.

Akizungumza moja kwa moja kutoka nchini Ivory Coast, mshambuliaji huyo alisema kuwa anakuja Tanzania rasmi kuanza kazi ya kuipambania Yanga huku akiamini kuwa atafanya vyema pia akiweka wazi shauku yake ya kuanza kukipiga ndani ya timu hiyo.

“Wananchi muda si mrefu nakuja Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha kuwa nawapa furaha, nafurahi kujiunga pamoja nanyi kwenye hii timu, naamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa hapa na tutafurahi pamoja,” alisema mshambuliaji huyo.

Previous articleMRC Kigamboni Yaishukuru Meridianbet
Next articleBOSI WA MAN CITY ATIMKIA MAN UTD KUWA CEO MPYA