KAZI KUBWA INAHITAJIKA KUFANYIKA KWA TANZANIA

    IPO wazi kwamba mashindano makubwa Afrika ambayo ni Kombe la Mabingwa Afrika, (AFCON) yanazidi kushika kasi na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ina kazi ya kusaka ushindi ikiwa kundi F.

    Kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Morocco ilipoteza Januari 17 kwa kushuhudia ubao ukisoma Morocco 3-0 Tanzania hivyo bado kuna mechi mbili mkononi ambazo ni muhimu kupata ushindi.

    Haikukuwa mechi nyepesi kutokana na kila timu kuhitaji ushindi lakini ni muda wa Stars kuonyesha kwamba mpira ni sayansi inayohitaji hesabu na kujituma bila kukata tamaa kwa mechi zinazofuata.

    Morocco sio timu ndogo ni moja ya timu imara zenye wachezaji wakubwa lakini inawezekana kuwa imara zaidi kwa mechi zinazofuata.

    Matokeo yanatafutwa ndani ya dakika 90 na sio kazi kubwa kushuhudia yule ambaye atapata maumivu ama kicheko mwisho hivyo kila mmoja atakuwa kwenye kibarua chake kupambania kombe.

    Muda ni sasa kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata matokeo chanya. Inawezekana kutokana na uwezo wa wachezaji ambao wameitwa kwenye timu ya taifa. Muhimu kushiriki kwa kuleta ushindani na sio kuwa wasindikizaji.

    Hakika ni wakati ambao ni mgumu kwa wachezaji kusaka ushindi dhidi ya timu ngumu lakini wote wanatumia dakika 90 uwanjani hivyo ni muda wa kupambana kufanya kweli mwanzo mwisho.

    Ni muda sasa wa kufanya kwenye kwenye kila mechi kwa kutafuta matokeo ili kuwatoa kimasomaso Watanzania ambao wanapenda kuona matokeo mazuri yanapatikana uwanjani

    Waliopewa jukumu hilo ni wachezaji waliopo kambini na mashabiki kuendelea kuwaombea wachezaji wafanye vizuri kwenye kila mechi ambazo watashuka uwanjani.

    Mwanzo mzuri utakuwa ni mwendelezo wa kufanya vizuri kwa mechi ambazo zinafuata kwa wakati huu na inawezekana kwa asilimia kubwa ikawe hivyo.

    Mashabiki wanapenda kuona ushindi ukipatikana na hilo halitokei kwa bahati mbaya ni lazima kila mmoja apambane kupata ushindi kwenye mchezo husika ambao utakuwa unachezwa.

    Muda wenyewe ni sasa na wachezaji wanatambua kwamba inawezekana kwa kuwa kupitia mazoezi ambayo wanafanya wanakuwa imara kwa ushindani kitaifa na kimataifa.

    Nidhamu kubwa inahitajika wakati wa maandalizi hii itaongeza uelewa kwa wachezaji. Kufanya vizuri kwenye mazoezi kutaleta mwendelezo mzuri mpaka eneo la mechi ambayo ni kumalizia kazi iliyoanza kutengenezwa mwanzo uwanja wa mazoezi.

    Majukumu ni mengi kwa kila idara na makosa yakiwa mengi ni rahisi kupoteza hivyo ni muhimu kupunguza makosa kwenye mechi ambazo zitachezwa uwanjani katika kusaka ushindi.

    Maelekezo kutoka kwa benchi la ufundi ni muhimu kufuatwa kwa umakini ili timu ipate matokeo mazuri baada ya mchezo. Yale makosa yaliyopita ni muda wake kufanya kazi sasa sehemu ya mchezo.

    Kupata matokeo uwanjani ni kutumia vizuri makosa ya timu pinzani huku. Wakati mnatumia makosa ya wapinzani ni muhimu kupunguza makosa kwa upande wenu.

    Hakuna timu inayoingia uwanjani ikiwa na hesabu za kushindwa hivyo ni muda wa kupambana kwa hali na mali kuwa kwenye mwendo mzuri.

    Namna ambavyo mtaanza kwenye mchezo wa mwanzo itakuwa mwendelezo kwenye mechi zinazofuata kwa kuwa hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho hivyo ni muda wa kufanya kweli.

    Previous articleAZAM FC WAMESHUSHA KITASA CHA KAZI
    Next articleNYOTA HUYU ALITAKIWA NDANI YA SIMBA