AFCON IWE NJIA YA KUTUSUA KIMATAIFA, KAZI IFANYIKE

    KADRI kila siku zinavyozidi kwenda wachezaji wanatambua namna ushindani ulivyo mkubwa kwenye mashindano husika. Ipo wazi kwa namna ambavyo mashindano yanazidi kuendelea hapo ndipo ugumu wake unaongezeka.

    Hatua moja inaleta hatua nyingine ambacho kinatakiwa kufanyika ni kwa kila hatua kuwa na mipango makini ambayo italeta matokeo mazuri hapo kesho.

    Ipo wazi kwamba ambacho kipo mbele kwa sasa kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, (Afcon) ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

    Januari 13 hadi 14  inatarajiwa kuanza kufanyika huko Ivory Coast ambapo kwa sasa ni siku kadhaa zinahesabiwa. Ikumbukwe kwamba kuna wakati ilikuwa ni miezi kadhaa inahesabiwa lakini kwa sasa zinahesabiwa siku.

    Inamaanisha kwamba jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa sasa linakwenda kutimia na kutimiza ule usemi wa subira yavuta kheri ambayo inakuja ni kheri lakini haitakuwa vizuri kama maandalizi yatakuwa mabovu.

    Kama maandalizi yatakuwa mabaya kwa timu hakuna miujiza kusubiri kuona matokeo mazuri uwanjani kwa kuwa ili upate ushindi ni lazima ufanye maandalizi mazuri.

    Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo itaweka kambi huko Misri nina amini wanatambua ugumu wa mashindano haya hivyo watajituma bila kuogopa.

    Kujituma kwa wachezaji sio siku ya mechi za ushindani pekee bali kwa sasa kuanzia kwenye mazeozi ni muhimu kuwa makini kwenye kufuata maelekezo ya benchi la ufundi na wachezaji kuongeza juhudi kwenye kuyatekeleza hayo maelekezo.

    Ikiwa wachezaji watashindwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ni rahisi kukwama kupata matokeo hapo kesho. Ili kupata matokeo mazuri ni muhimu kufanya kweli sasa kwenye maandalizi kuelekea mashindano husika.

    Kambi isiwe sehemu ya kufanya utalii wa ndani kwa wachezaji bali iwape hasira kufanya kweli kwenye mechi zote za ushindani kwa kuwa kila kitu ambacho kinafanyika huko ni gharama.

    Gharama ya uwekezaji ambayo inafanywa ni muhimu kulipwa kwa vitendo kwenye mechi za ushindani kwa kupata matokeo mazuri uwanjani na inawezekana.

    Ukweli ni kwamba kila mchezaji ana uwezo mkubwa kutokana na kipaji alichonacho hivyo kinachotakiwa ni kuona namna gani kipaji hicho kinatumiwa.

    Jambo lingine la msingi ni kuzingatia nidhamu kwenye maelekezo ambayo yatakuwa yanatolewa pamoja na kufuata ratiba zote zinazotolewa kutoka wa benchi la ufundi.

    Kupata nafasi kupeperusha bendera ya timu ya Taifa kimataifa ni jambo kubwa ambalo linapaswa litumike kwa ukubwa wake kwenye mechi zote na kupata matokeo mazuri.

    Haya mashindano yafungue njia kwa wachezaji pia kuongeza thamani yao sokoni ili kupata timu za nje ambazo zitakuwa zikifuatilia mashindano haya.

    Huu ni mlango mwingine wa fursa ambayo imekuja kwa mtindo wa kazi ya taifa hivyo ni muhimu kuangalia namna gani itakuwa faida na sio hasara kwa mchezaji.

    Kupata dili la kwenda nje kucheza ama soka la kulipwa mbali na Bongo sio ngumu wala sio rahisi bali ni kujituma kwa mchezaji husika na kutumia nafasi ambayo ataipata kwenye timu husika.

    Watakaojituma bila kuogopa kwenye Afcon hii watavuna matunda ya kile wanachokitumikia kwa sasa na yote haya yaanzia kwenye mazoezi kuelekea kwenye mechi husika.

    Hakuna ambaye ni fungu la kukosa kila siku, ikiwa ipo siku ya kukosa basi na siku ya kupata ipo ikawe hivho kwenye mashindano ya safari hii ambayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

    Yote kwa yote Afcon iwe daraja la kuwapeleka kwenye anga la kimataifa wachezaji husika na kuwa kwenye ulimwengu mwingine kuipeperusha bendera ya Tanzania.

    Kazi ni kubwa na kila mmoja anapaswa kufanya hayo kwa kujituma katika kutekeleza majukumu yake kwa wakati bla kusukumwa na mwingine.

    Kuzingatia nidhamu kutaongeza nguvu kwa wachezaji kucheza kwa ushirikiano mkubwa uwanjani na hakuna ambaho kitakwenda tofauti kwenye haya yote, hivyo yu basi.

    2024 ikawe ni kheri kwa kila mmoja na kwa wale ambao wanamatatizo tunawaombea kheri kwa Mungu warejee kwenye ubora wao na kuendelea na majukumu ya kulijenga taifa.

    Vist Temeke

    Previous articleCRIS JABAR MWAMBA ANAYEWAZA KITAIFA NA KIMATAIFA
    Next articleMWAKINYO: SINA HOFU NA MABONDIA WENYE MIILI WALA PIKO