Home Sports MWAKINYO: SINA HOFU NA MABONDIA WENYE MIILI WALA PIKO

MWAKINYO: SINA HOFU NA MABONDIA WENYE MIILI WALA PIKO

BONDIA Hassan Mwakinyo ametoa maneno ‘mbofumbofu’ kwa kueleza kwamba haogopi mabondia wenye miili mikubwa na pia huwa anafurahia kuona ‘piko’ anazojichora bondia huyo.

Huo ni mkwara kwa moja ya mabondia Bongo ambao wana michoro kwenye miili pamoja na kuwa na umbo kubwa.

Mkwakinyo karusha jiwe gizani ambapo hajamtaja bondia ambaye wamekuwa wakiingia kwenye vita ya maneno mara kwa mara, kila mmoja akimtambia mwenzake.

“Siogopi mabondia wenye miili mikubwa ama michoro kwenye miili yao sina hofu katika hilo nipo imara,”.

Previous articleAFCON IWE NJIA YA KUTUSUA KIMATAIFA, KAZI IFANYIKE
Next articleKASINO YA ZORBAS TAVERN INAKUPA USHINDI X10,000 YA DAU LAKO