UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa kwenye mpango wa usajili utaongeza mkata umeme wa kazi mithili ya Fabrince Ngoma ili kuongeza uimara kwenye timu hiyo.
Ipo wazi kwamba Simba kwa msimu wa 2023/24 haijawa bora kwenye eneo la ulinzi na ushambuliaji huku eneo la ukabaji ikiwa na wachezaji wa kazi kama Fabrince Ngoma, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema ikiwa watakwenda kufanya usajili kwenye kila idara kuna aina ya wachezaji ambao wanapaswa kuwa katika usajili huo.
“Maboresho ya kikosi ni muhimu lakini lazima kuzingatia vigezo ambavyo ni muhimu kuwa kwenye timu yetu kikubwa ni kuona kwamba wachezaji wanapata nafasi ya kucheza katika timu.
“Kwenye eneo la mkata umeme tutamleta mtu kama Ngoma unaona kazi yake ni kubwa na anafanya kweli hivyo mashabiki wasiwe na hofu tunaamini tutafanya vizuri,” amesema.
Timu hiyo inashiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar ambapo inatarajiwa kuelekea visiwani Desemba 30 .