Home Sports NAMUNGO WANA JAMBO LAO HUKO

NAMUNGO WANA JAMBO LAO HUKO

UONGOZI wa Namungo FC umeeleza ukimya unaoendelea kwao ni mchakato wa kukimbizana na dirisha dogo la usajili ili waweze kufanya jambo litakaloendelea kuwapa mashabiki wao furaha zaidi.

Timu hiyo kwa sasa inanolewa na aliyekuwa kocha wa viungo Shadrack Nsajigwa baada ya Denis Kitambi kupewa Thank You anatajwa kuibukia Geita Gold baada ya Hemed Morroco kubwaga manyanga.

Namlia Kindamba,  amesema:-“Kocha Nsajigwa anaendelea na majukumu yake na anajua uwezo wa wachezaji wetu na kipi tunakihitaji kwenye ligi hivyo palipo na mapungufu yatafanyiwa kazi mashabiki wasiwaze muda bado upo wa sisi kufanya jambo,” alisema Kindamba.

Namungo FC inashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 17 na  tayari imeshacheza michezo 13 msimu wa ligi 2023/24.

Previous articleANAKUJA YANGA WINGA HUYU WA DR CONGO
Next articleONANA WA SIMBA ATAJA SIRI YA MAFANIKIO