Home Sports ONANA WA SIMBA ATAJA SIRI YA MAFANIKIO

ONANA WA SIMBA ATAJA SIRI YA MAFANIKIO

WILLY Onana kiungo mshambuliaji wa Simba amesema ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzake ndani ya kikosi ni sababu iliyowapa nguvu wakashinda.

Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Desemba 19 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-0 Wydad Casablanca na mabao yote yalifungwa na Onana.

Onana alifunga mabao hayo akitumia pasi za kiungo rasta, Kibu Dennis dakika ya 36 na 37 yakatosha kuipa pointi tatu Simba.

“Kila kitu ambacho tunafanya ni kwa ushirikiano na hilo linatupa nguvu kupata matokeo uwanjani hivyo mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi kwa ajili ya kuona tunakuwa kwenye mwendo mzuri.

“Tunatambua kwamba matokeo mazuri ni kitu ambacho kinahitajika na inapaswa kuwa endelevu kwenye kila mechi,” amesema.

Previous articleNAMUNGO WANA JAMBO LAO HUKO
Next articleYANGA YAKATAA UTEJA WA MIAKA 25 LIGI YA MABINGWA, PACOME ATAJWA