Home Sports SIMBA YAAMBULIA SARE TENA UGENINI

SIMBA YAAMBULIA SARE TENA UGENINI

WAWAKILISHI wa Tanzania Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wameambulia sare ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Ni sare ya pili leo wanapata katika hatua ya makundi baada ya mchezo wa kwanza kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya ASEC Mimosas mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ngoma ni nzito kwa Simba kwenye hatua ya makundi dakika 180 wamekusanya pointi mbili wakipoteza pointi nne.

Katika mchezo wa leo mshambuliaji Jean Baleke alikosa utulivu kumalizia nafasi wanazopata huku kona zilizopigwa na Saido Ntibanzokiza zote zikiwa hazina faida kwao.

Previous articleJWANENG 0-0 SIMBA
Next articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AL AHLY