USHINDANI KWENYE LIGI KUU BARA UENDELEE

MZUNGUKO wa kwanza bado unaendelea kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara. Ikumbukwe kwamba kwa sasa timu nyingi zinapambana kufanya vizuri na kupata matokeo ndani ya uwanja.

Kila timu inafanya vizuri ndani ya dakika 90 kusaka ushindi. Kushindwa kufanya vizuri kwenye mechi husika haina maana kwamba kazi itakuwa imekwisha hapana ni muhimu kupambana zaidi kwa mechi zinazofuata.

Wale ambao wanashindwa kupata ushindi ni muhimu kufanyia kazi makosa yao ili kupata kile wanachokistahili kwenye mechi zinazofuata. Bado inawezekana kwa timu kupata matokeo ndani ya uwanja kutokana na ushindani uliopo.

Muda ni sasa kufanyia maboresho ya kile ambacho mnafundishwa uwanjani. Hakuna mwalimu ambaye anafundisha kuwachezea faulo wengine uwanjani hivyo huwa ni hulka kwa wachezaji.

Wachezaji wanapaswa kuongeza nidhamu kwenye mechi zote ili kupata kile wanachokitafuta. Ushindani ni mkubwa na kila mmoja anapaswa kuendelea kupambana kusaka ushindi.

Mechi zina ushindani mkubwa na kila mchezaji anapenda kuona timu inapata ushindi. Kupata matokeo ni maandalizi mazuri na kinachotakiwa ni kutumia makosa ya wapinzani.

Mashabiki wanapenda kuona kila ambacho kinapatikana uwanjani kinawapa furaha hata wachezaji wao wanaowapenda wanafurahi kuwaona wakitimiza majukumu yao.

Kuumia kwa wachezaji kutokana na kuchezewa faulo ndani ya uwanja hili linapaswa lipungue kabisa na mpira uchezwe kwa umakini kila wakati kwenye mechi zote za ugenini na nyumbani.

Ni muda kuwa makini katika kutimiza majukumu huku wachezaji wakilindwa kwa umakini. Muda ni sasa kila mchezaji kupunguza matumizi ya nguvu zisizo za lazima.

Hiyo itafanya muda wa mavuno kila mmoja kupata kile ambacho anastahili kwa kuwa ligi ni ngumu na wachezaji lazima wawe fiti kuendeleza upinzani ndani ya uwanja.

Kwa timu zote shiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na Championship kwenye mzunguko wa kwanza ni muhimu kufanya kazi kubwa kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.

Kikubwa ambacho kinawafanya wamalize vizuri ni ule mwendelezo wa kujiamini. Kushinda mchezo mmoja kunaongeza hali ya kuendelea kupambana kwa ajili ya mechi inayofuata.

Licha ya kwamba mchezo wa mpira ni maalumu kwa ajili ya makosa bado kuna nafasi ya kufanyia kazi makosa yenyewe. Kila mmoja anapenda kuona anapata matokeo chanya akiwa uwanjani.

Kila timu kwa nafasi yake inakazi ya kuangalia wapi ilifanya makosa kwenye mechi zilizopita ili kupata ushindi kwenye mechi zinazofuata.

Mechi ni ngumu na kila timu inapambambana kupata matokeo chanya. Mzunguko wa kwanza unakuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa kila mchezaji anahitaji kuonyesha uwezo alionao.

Hapo ndipo inatokea timu zinakuwa kwenye kasi mbaya kuendelea kuwa kwenye mwendo huo na zile ambazo zilianza vizuri kuendelea kupata matokeo mazuri.

Muda ni sasa kwa kuwa mzunguko wa kwanza unaendelea kwa timu ambazo hazijawa na mwendo mzuri kurekebisha mapungufu yao.

Ni ngumu kupata matokeo mazuri ikiwa hakutakuwa na maandalizi bora. Makosa yaliyopatikana kwenye mechi zilizopita ni muhimu kufanyiwa kazi mapema ili kuyapunguza kwa mechi zijazo.

Kila kitu kinawezekana na ushindani mkubwa kwenye ligi ya ndani unaongeza thamani ya ligi yetu pamoja na wachezaji kuongeza thamani kwenye soko kitaifa na kimataifa.